Sunday, 7 September 2014

KAMA BADO HUJAIONA VIDEO MPYA YA MR NAY YA NEY WA MITEGO



jipatie huduma bomba sana na za hali ya juu kuhusu kila kitu kwenye cover hapo juu wakionesha , ni wakali kwa huduma mbalimbali tu hasa graphics design na music production.

DOWWNLOAD HAPA   VIDEO YA NAY WA MITEGO
http://www.youtube.com/watch?v=uS2uXrCVe6s

Sunday, 31 August 2014

ARSENAL REKODI YAO DHIDI YA LEICESTER, TABLE YA LIGI YA UINGEERZA NA PIA MATCHDAY LIVE TABLE HAPO CHINI

rekodi fupi ya arsenal dhidi ya leicester city kwa muda ambao walishakutana , ambapo leo watakutana dimbani pale arsena l fc watakuwa wageni kwa leicester city 

msimamo wa ligi kuu ya uingereza mpaka sasa CHELSEA FC ikiongoza ligi baada ya kutoa kichapo cha adabu kwa wakali wao wa muda mfupi EVERTON FC 

picha ya hapo juu inaosha ni jinsi gan pale uwanaja wa spurs utakuwa mgumu baada ya timu mbili matata kungoana meno , huku ASTON VILLA wakichuana na HULL CITY

Saturday, 23 August 2014

DIAMOND ATANGAZAA .....>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>


Diamond na Wema wamekuwa katika mahusiano ya muda mrefu, wakiachana na kurudiana.
Diamond na Wema wamekuwa katika mahusiano ya muda mrefu, wakiachana na kurudiana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa.
Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’
“Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza.
Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu”

Atletico beat Real to clinch Super Cup

Atletico Madrid © Action Images
Atletico Madrid gained some measure of revenge for their Champions League final defeat to Real Madrid by beating their city rivals 1-0 at the Vicente Calderon on Friday to win the Spanish Super Cup 2-1 on aggregate.
The hosts made the best possible start as Mario Mandzukic volleyed home the winner from Antoine Griezmann's pass after just 90 seconds.
Real boss Carlo Ancelotti had named Cristiano Ronaldo on the bench due to the effects of a hamstring injury that had seen him withdrawn from the first leg.
However, even the Portuguese couldn't break down Atletico's typically well-organised defence as they held on to end Real's hopes of claiming six trophies this season.
As well as leaving Ronaldo on the bench, Ancelotti also fuelled speculation over Angel di Maria's future by excluding the Argentine from his squad entirely.
Real were caught out by a flying start from Atletico as Raphael Varane's misjudged header allowed his French international teammate Griezmann to feed Mandzukic to score his first goal since signing from Bayern Munich.
The visitors slowly grew into the game, though, and Luka Modric was inches away from a spectacular equaliser when he volleyed just over from outside the area.
James Rodriguez then began to dictate the pace of the game and he was only denied a leveller by a spectacular save from Miguel Angel Moya before the Colombian also directed a header just wide of the target.
Atletico boss Diego Simeone was sent-off for protesting that right-back Juanfran hadn't been allowed back onto the field quickly enough after receiving treatment for a facial injury.
And the Argentine could be in for a severe ban as he confronted the assistant referee and sarcastically applauded the decision.
Rodriguez then fed Gareth Bale inside the area, but the Welshman pulled his shot disappointingly wide.
However, it was Atletico who had the clearest chance to double their advantage before halftime as Raul Garcia inexplicably headed over Koke's corner from point-blank range.
Ronaldo made his entrance at the break as he replaced the ineffective Toni Kroos.
Garcia was inches away again at the start of the second period as this time he turned a Koke free-kick onto the underside of the bar and Iker Casillas reacted well to prevent Mandzukic forcing the ball home from close range.
And Garcia was desperately unlucky again moments later as this time he fired just wide with Casillas beaten.
Ronaldo made his first real impression with a thunderous effort that was well held by Moya, but Atletico were creating the greater threat and went close twice more through Koke and Griezmann.
Real's miserable evening was rounded off in stoppage time as Modric was sent off for a second bookable offence when he upended Cristian Rodriguez.

Jose Mourinho admits that Petr Cech is not happy at Chelsea


Cech could leave Stamford Bridge this summer. Read more Chelsea transfer rumours. Jose Mourinho has admitted that Chelsea goalkeeper Petr […]
Cech could leave Stamford Bridge this summer.
Jose Mourinho has admitted that Chelsea goalkeeper Petr Cech is not “totally happy” at Stamford Bridge after being dropped for Thibaut Courtis, fulling speculation that the experienced stopper could leave the club this summer.
Cech lost his place as the club’s long-serving first choice for the Blues’ opening Premier League victory at Burnley, and Courtois’ performance suggested that he is likely to keep his place.

Friday, 22 August 2014


Afisa wa shirika la afya duniani aeleza kuhusu janga la Ebola Duniani
Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.

Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.
Wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki.
Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia.
Nigeria ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani Afrika na ndio ya hivi karibuni kuripoti kuwa na thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni.
Serikali hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka Afrika Magharibi.

Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini Nigeria.

Wednesday, 20 August 2014

AJALI HIZI, MENGI HUTOKEA

Ndege ya shirika la ndege ya malaysia wakati wa uhai wake.
Ofisa mmoja mwanamke mwenye cheo cha juu katika bankkubwa iliyoko mjini Kuala Lumpur , Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba mamilioni ya dola za kimarekani kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege iliyopotea ya Malaysia Air Line MH370 ambayo ilipotea katika mazingira ya kutatanisha,katika bahari ya Hindi mapema mwezi March.
Pamoja na kushtakiwa huko, mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine yapatayo 16 kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.
Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kupoka pesa.
Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia Air Line.

SOMA HOTUBA YA MWISHO YA KANALI MUAMAR GHADAFI KABLA HAJATANGULIA MBELE YA HAKI! MY HERO SALUTE!!

Hotuba ya Mwisho ya Kanari Muammar Gafafi enzi za uhai wake,watanzania tunalojambo la kujifunza.
Alianza hivi,

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu
(Allah), Mungu mpaji, na mwenye
rehema....


Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa
zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni
kuwa nilifanya kila nilichoweza
kuwapa watu wangu nyumba,
hospitali na shule. Na kila walipohisi
njaa niliwapa chakula. Niliifanya
Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi
nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya Ronald
Regan (Rais wa zamani wa
Marekani), alipomuua binti yangu
niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua
mimi lakini akamuua yule binti yatima
masikini. Niliwasaidia kaka na dada
zangu waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya
watu wangu waelewe maana halisi
ya demokrasia; ambapo watu wa
tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa
na nyumba ya vyumba kumi, nguo
mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika.
Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi
walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia
Marekani kuwa wanataka
"demokrasia" na "uhuru". Hawakujua
kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua
ni mfumo wa unyonyaji ambapo
mbwa mwenye nguvu zaidi huwala
mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni.
Walitaka "demokrasia". Wakasahau
kuwa hata Marekani hakukuwa na
huduma za afya za bure, dawa bure,
elimu bure na chakula cha bure.
(Huduma hizi za bure zilipatikana
Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara
hana cha bure. Labda awe
ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani
bado hawakuridhika. Lakini wapo
waliojua mimi ni mtoto wa Gamal
Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi
na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi
kuwa nae tangu enzi za Salah-al-
Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa
Suez kwa watu wake nami nilikua
naipigania Libya kwa watu wangu.
Nilikua najaribu kufuata nyayo zake
ili kuwaweka watu wangu huru
kutoka kwenye makucha ya wakoloni
wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati
ya majeshi makubwa ya dunia katika
historia. Mwanangu mpendwa
mwenye asili ya Afrika, Obama
anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki
yetu ya huduma za bure za afya,
huduma za bure za elimu, na chakula
chetu; na kutuletea mfumo mpya wa
kimarekani wa kuiba uitwao
"Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu
tunajua maana yake. Maana yake ni
kuwa "washirika" wanatawala
mataifa, wanatawala dunia, na watu
wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu.
Lazima niwe na msimamo. Na kama
Mungu atapenda nitakufa kwa
mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu
kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula
bora, na huduma bora za afya.
Mapenzi ya Allah yaliyowezesha
tukawasaidia kaka na dada zetu
waafrika na waarabu waliokuwa na
shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili
kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu
wangu, na wengine ambao ni kama
wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa
dunia kuwa nilisimama kupinga
uvamizi wa NATO. Nilisimama
kishujaa kupinga usaliti wa nchi za
magharibi na nia mbaya za kikoloni.
Na hapa nimesimama na ndugu
zangu waafrika, kaka na dada zangu
waislamu kama ngao yangu ya
matumaini.
Wakati wengine walipokuwa
wanajenga majumba ya kifahari,
mimi niliishi kwenye nyumba ya
kawaida na kwenye mahema. Siwezi
kusahau maisha yangu ya utoto kule
Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu
kipumbavu. Na kama alivyokua
Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika
uislamu, nilichukua kidogo sana kwa
ajili yangu, na sehemu kubwa
niliwapa wananchi.
Watu wa magharibi wameniita
"kichaa", "mwendawazimu" lakini
wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa
wala mwendawazimu; ila waache
waendelee kudanganya. Wanajua hii
ardhi ni huru na haipo kwenye
himaya ya kikoloni. Huu ndio
msimamo wangu na dira yangu na
imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya
mwisho ili watu wangu wawe huru.
Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki
waaminifu na tuwe huru.

-- Mu'uammar Qaddafi.

Azuiwa kuingia Dubai akihofiwa kuwa mchawi

Uso wake Rolf Bushholz ulivyo na maumbile kama pembe
Mwanaume mmoja kutoka Ujerumani anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu aliyetoboa zaidi mwili wake, Rolf Buchholz amekatazwa kuingia Dubai.
Rolf Buchholz, ametoboa mwili wake mara 453 ikiwemo usoni mwake na ana pembe mbili juu ya paja la uso wake.

Rolf Bushholz aliyenyimwa ruhusa ya kuingia Dubai.
Bwana Buchholz alieleza BBC kuwa maafisa wakuu katika uwanja wa ndege walihofia huenda alikuwa ni '' mchawi'' .Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa ameratibiwa kuandaa onyesho katika klabu moja mjini humo.
Mtaalamu huyu wa tarakilishi alitambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness, kama mwanaume aliyetoboa mwili wake zaidi duniani mwaka wa 2012.

Rolf Bushholz katika moja ya maonyesho yake
Alieleza wanahabari wa Press News Agency kuwa hapo awali alikuwa amekubalika lakini baadaye akarejeshwa kabla ya kufika eneo la maafisa wa usafiri ndipo akarejeshwa katika ndege iliyokuwa ikielekea mjini Instabul Uturuki.
Onyesho lake katika mgahawa maarufu wa Irque le Soir ulioko katika hoteli ya Fairmont Hotel Dubai lilifutiliwa mbali.

Mdomo wake uso wake Rolf Bushholz ulivyotogwa
Maafisa wa mgahawa huo wa Fairmont Dubai wamesema kuwa walifanya chochote kadri ya uwezo wao kumuingiza Buchholz nchini Dubai lakini hawakufua dafu.
Bwana Rolf amesema kuwa mizigo yake bado iko Dubai na aliapa kwenye mtandao wa kijamii kuwa hatarudi tena katika milki za Kiarabu.
Polisi na Maafisa wa usafiri wa ndege nchini Dubai hawajazungumzia swala hilo.

DOWNLOAD HAPA NGOMA YA CHIDBEENZ FT DIAMOND , AY


NI VYEPESI KULIKO UNAVYOFIKIRI
CHIDBEENZ FT DIAMOND , AY _ MPAKA KUCHEE

Thursday, 14 August 2014

EBOLA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI


Afisa wa shirika la afya duniani aeleza kuhusu janga la Ebola Duniani
Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.

Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.
Wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki.
Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia.
Nigeria ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani Afrika na ndio ya hivi karibuni kuripoti kuwa na thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni.
Serikali hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka Afrika Magharibi.

Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini Nigeria.

MWANAUME ANASWA NA UNGA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE BONGO HUYU HAPA LIVE!!


Hati ya kusafiria ya mtuhumiwa huyo yenye namba AP816263 iliyotolewa Julai 3,2014 nchini Columbia. (picha: Francis Dande)

Raia wa Colombia, Andres Filipe Ballesteros Uribe (28), alikamatwa Jumatatu iliyopita katika uwanja wa ndege Dar Es Salaam baada ya kukutwa na cocaine. Mkuu wa kikosi hicho, Kamanda Godfrey Nzowa alisema mtuhumiwa huyo aliingia nchini saa nane usiku kwa ndege ya shirika la Ethiopian akitokea Adisi Ababa.

Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na cocaine iliyofungwa kwenye pakiti sita tofauti na kuiweka sehemu za siri, kiunoni kama mkanda na nyingine tumboni.Kamanda Nzowa alisema mtuhumiwa huyo mwenye pasi ya kusafiria namba AP816263 iliyotolewa Julai 3,2014 nchini Colombia, alitoka Colombia kupitia Addis Ababa kuja Tanzania huku akibainisha kwamba hiyo ni njia mpya ya usafirishaji wa dawa hizo haramu.

“Hawa jamaa wanajaribu kubuni mbinu mpya kama huyu kijana alikuwa amefunga unga wa cocaine kama zilivyokuwa zikifungwa pipi na akazimeza… mpaka sasa ameshatoa pipi 13 kwa njia ya haja kubwa na anaendelea kutoa. …Sio rahisi kujua idadi ya mzigo aliokuwa nao mpaka atakapomaliza kuzitoa zote za tumboni ndiyo tunaweza kusema uzito wa dawa hizo na thamani yake,” alisema kamanda Nzowa.



Baadhi ya dawa ambazo mtuhumiwa alikuwa amezimeza.

Alisisitiza kwamba taarifa sasa wanazopeana kwenye mtandao wao unawezesha kukamatwa kwa watuhumiwa huku akibainisha kuwa lengo ni kudhibiti usafirishaji kwa njia yoyote. Nzowa alisema Felipe aliwasili kwa ndege ya Ethiopia Airlines akitokea kwao, Colombia, kupitia Ethiopia.

"Baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema, polisi wa JNIA na vijana wa kikosi changu, walimfuatilia hadi alipotua. Tulimweka chini ya ulinzi, katika mahojiano ndipo alipoonyesha dawa hizo. Kwa kadiri anavyoendelea kuzitoa tumboni, tunadhani zinaweza kuwa zaidi ya gramu 800. Tunamshikilia na mahojiano yanaendelea," alisema Nzowa.



Suruali ya mtuhumiwa ikiwa imezunguzishiwa cocaine.
Hata hivyo, mahojiano kati ya polisi na Felipe yamekumbwa na tatizo la lugha, kwani jeshi hilo halikuweza kupata mkalimani mara moja ambaye angesaidia kupata taarifa za kina za mtuhumiwa huyo na wengine wa kigeni wanaokamatwa uwanjani hapo na kubaini mtandao mzima. "Itatuchukua muda sana kumuhoji kwa sababu anazungumza Kihispanyola. Tunafanya juhudi kupata wakalimani," alisema Nzowa.

Kamishna Msaidizi wa Polisi uwanjani hapo, Hamis Selemani alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, akisema, ameshaanza kutoa tumboni dawa alizozimeza.


Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa akionesha Cocaine zilizokuwa zimefichwa katika mkanda wa suruali aliyokuwa amevaa raia wa Colombia, Andres Filipe Ballesteros Uribe (28), mara baada ya kukamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (picha: Francis Dande)

Kamanda Nzowa alisema mafanikio yanaonekana kwa vile kuanzia Juni 24 mwaka huu hadi Agosti 10 hakuna mtu aliyekamatwa akiingiza huku akibainisha kwamba umadhubuti wa mtandao wao umefanikisha hilo. “Asiyeamini kwamba tumefanikiwa atujaribu aone… naamini tunakokwenda dawa za kulevya hasa cocaine na heroine zitakuwa hazipiti wala kuingia Tanzania,” alisema na kuongeza kwamba wanadhibiti pia ulimaji wa bangi. Kwa mujibu wa kamanda huyo lengo la mtandao wao ni kudhibiti sio kukamata wala kuteketeza