Wednesday, 20 August 2014

SOMA HOTUBA YA MWISHO YA KANALI MUAMAR GHADAFI KABLA HAJATANGULIA MBELE YA HAKI! MY HERO SALUTE!!

Hotuba ya Mwisho ya Kanari Muammar Gafafi enzi za uhai wake,watanzania tunalojambo la kujifunza.
Alianza hivi,

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu
(Allah), Mungu mpaji, na mwenye
rehema....


Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa
zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni
kuwa nilifanya kila nilichoweza
kuwapa watu wangu nyumba,
hospitali na shule. Na kila walipohisi
njaa niliwapa chakula. Niliifanya
Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi
nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya Ronald
Regan (Rais wa zamani wa
Marekani), alipomuua binti yangu
niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua
mimi lakini akamuua yule binti yatima
masikini. Niliwasaidia kaka na dada
zangu waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya
watu wangu waelewe maana halisi
ya demokrasia; ambapo watu wa
tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa
na nyumba ya vyumba kumi, nguo
mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika.
Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi
walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia
Marekani kuwa wanataka
"demokrasia" na "uhuru". Hawakujua
kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua
ni mfumo wa unyonyaji ambapo
mbwa mwenye nguvu zaidi huwala
mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni.
Walitaka "demokrasia". Wakasahau
kuwa hata Marekani hakukuwa na
huduma za afya za bure, dawa bure,
elimu bure na chakula cha bure.
(Huduma hizi za bure zilipatikana
Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara
hana cha bure. Labda awe
ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani
bado hawakuridhika. Lakini wapo
waliojua mimi ni mtoto wa Gamal
Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi
na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi
kuwa nae tangu enzi za Salah-al-
Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa
Suez kwa watu wake nami nilikua
naipigania Libya kwa watu wangu.
Nilikua najaribu kufuata nyayo zake
ili kuwaweka watu wangu huru
kutoka kwenye makucha ya wakoloni
wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati
ya majeshi makubwa ya dunia katika
historia. Mwanangu mpendwa
mwenye asili ya Afrika, Obama
anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki
yetu ya huduma za bure za afya,
huduma za bure za elimu, na chakula
chetu; na kutuletea mfumo mpya wa
kimarekani wa kuiba uitwao
"Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu
tunajua maana yake. Maana yake ni
kuwa "washirika" wanatawala
mataifa, wanatawala dunia, na watu
wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu.
Lazima niwe na msimamo. Na kama
Mungu atapenda nitakufa kwa
mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu
kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula
bora, na huduma bora za afya.
Mapenzi ya Allah yaliyowezesha
tukawasaidia kaka na dada zetu
waafrika na waarabu waliokuwa na
shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili
kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu
wangu, na wengine ambao ni kama
wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa
dunia kuwa nilisimama kupinga
uvamizi wa NATO. Nilisimama
kishujaa kupinga usaliti wa nchi za
magharibi na nia mbaya za kikoloni.
Na hapa nimesimama na ndugu
zangu waafrika, kaka na dada zangu
waislamu kama ngao yangu ya
matumaini.
Wakati wengine walipokuwa
wanajenga majumba ya kifahari,
mimi niliishi kwenye nyumba ya
kawaida na kwenye mahema. Siwezi
kusahau maisha yangu ya utoto kule
Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu
kipumbavu. Na kama alivyokua
Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika
uislamu, nilichukua kidogo sana kwa
ajili yangu, na sehemu kubwa
niliwapa wananchi.
Watu wa magharibi wameniita
"kichaa", "mwendawazimu" lakini
wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa
wala mwendawazimu; ila waache
waendelee kudanganya. Wanajua hii
ardhi ni huru na haipo kwenye
himaya ya kikoloni. Huu ndio
msimamo wangu na dira yangu na
imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya
mwisho ili watu wangu wawe huru.
Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki
waaminifu na tuwe huru.

-- Mu'uammar Qaddafi.

No comments:

Post a Comment