|
Waombolezaji wakitoa heshima zao huku wengine wakichukua picha za kumbukumbu
|
|
Mhubiri aliyejitolea baada ya kanisa la Rc kususa kuendesha misa |
|
Marehemu enzi za uhai wake |
|
Kijana wa boda boda akifurahia kuwapokonya chepe wenzake |
|
Vijana wakizichapa ngumi kugombea kuzika |
|
Dereva wa bajaji iliyobeba mwili wa marehemu |
|
Kijana aliyejitolea kuendesha ibada ya mazishi kulia akisaidiana na ndugu kuweka msalaba |
|
Mwakilishi wa kundi la Mundu Sanaa Group Bw Lackson akiweka shada la maua |
|
Mwenyekiti wa chama cha boda boda Iringa Joseph Mwambope akiweka shada la maua |
|
Huyu ndie kada wa Chadema aliyepewa nafasi ya kuweka shada na kuambilia kuzomewa |
Mwenyekiti wa chama cha boda boda na Bajaji Iringa Joseph Mwambope akizungumza katika mazishi hayo
............................................
MATUMAINI
ya vijana dhidi ya chama demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya
Iringa mjini imeanza kutoweka baada ya jana dereva boda boda zaidi ya
200 kuwazuia viongozi wa Chadema kupeperusha wala kufunika bendera
za chama hicho katika bajaji iliyobeba mwili wa dereva mwenzao Abisai
Mdesa .
Vuta
nikuvute hiyo ilitokea majira ya saa 4 asubuhi baada ya makada wa
Chadema kufika Chumba cha maiti katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Iringa wakiwa na bendera za Chadema kwa ajili ya kuwapa madereva wa
boda boda pamoja na kufunga katika bajaji iliyopaswa kubeba mwili wa
marehemu huyo bado bado msimamo wa boda bado ulionekana kupingana na
matakwa ya viongozi hao.
Vijana
hao walionesha kupinga msimamo wa makada hao wa Chadema kutoka
kufunika bendera wa chama chao katika jeneza la marehemu huyo wala
kupeperusha bendera ya chama chao katika msafara wa mazishi kwa madai
kuwa chama hicho cha boda boda Iringa si chama cha kisiasa na wala
hakina ubia na Chadema .
Wakizungumza
kwa jazba vijana hao waendesha boda boda boda walisema kuwa
wamesikitishwa na kitendo cha Chadema kutaka kujipatia umaarufu kupitia
mazishi ya dereva mwenzao huyu hali wakitambua kuwa wao si sehemu
ya Chadema.
Walisema
walikuwa tayari kuwashambulia kwa kipigo makada hao wanne wa Chadema
waliofika na bendera hizo iwapo wangeshindwa kuwasikiliza na
kuendelea na msimamo wao wa kufunga bendera.
Mwenyekiti
wa chama cha boda boda na Bajaji mjini Iringa Joseph
Mwambope aliwaeleza waandishi wa habari kuwa hatua ya Chadema kutaka
kujimilikisha msiba huo ni kosa kubwa na kuwa wanachotambua kuwa
marehemu hakuwa kiongozi wa Chadema ila alikuwa ni mwanachama wa chama
cha boda boda hivyo mbali ya ndugu mwenye nafasi ya kuendesha mazishi
hayo ni chama cha boda boda na Bajaji pamoja na wasanii wenzake wa
Mundu Sanaa Group na sio chama chochote cha siasa.
"Tunaomba
ieleweke kuwa chama cha boda boda si chama cha kisiasa hivyo
haturuhusu Chadema ama CCM kuja na bendera za vyama vyao katika msiba
huu japo hatuwakatazi kuja na magari yao yakiwa na bendera za vyama
vyao ila sio kuleta bendera tufungi kwenye boda boda na bajaji zetu
"alisema Mwambope
Kuwa
imekuwa ni kawaida ya Chadema na vyama vingine kujipendekeza katika
misiba ambayo wanahisi ina waombolezaji wengi ili kutumia nafasi hiyo
kujitangaza kisiasa ila wakati wa kuuguza vyama hivyo huwa havitokei
kuuguza.
"Huyu
mwenzetu mbali ya kupata ajali ya pikipiki kwa siku zaidi ya nne sasa
alikuwa amelezwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na madereva
tulianza kuchangishana ili kumfanyia rufaa kwenda Hospitali ya Taifa
Muhimbili .....sasa kama Chadema ambao leo wanakuja na bendera wapo
kwanini wasingetoa usafiri wa kwenda Muhimbili kama si kutaka kuonekana
sasa baada ya kifo"
Katika
hatua nyingine vijana hao wa boda boda walilazimika kuzomea kada wa
Chadema aliyepewa kuweka shada kaburini kutokana na kushindwa
kukabidhi ahadi yao ya mchango wa shilingi 25000 ambazo waliahidi kwenye
daftari la waombolezaji bila kutoa pesa hiyo .
No comments:
Post a Comment