Producer
wa wimbo mpya wa Ben Pol, ‘Unanichora’, Fundi Samwel ambaye ni raia wa
Sweden, amethibitisha kuachana na mke wake, Saraha.
Mtayarishaji huyo amesema sababu kubwa ya kuachana ni ubusy waliokuwa nao
uliosababishwa na muziki na hivyo kuwafanya wasiwe karibu kwa kipindi
kirefu.
“Mimi
na Saraha tuliachana, kilikuwa kitu kibaya kwangu na kwake pia ndio
maana nilikuwa kimya kidogo mwaka huu sababu unajua moyo ulivunjika sana
na mood lazima ipotee,” Fundi Samwel amemuambia Sam Misago kwenye
kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio.
“Unajua
kukaa na kufanya muziki lazima utumie muda sana na unatumia akili sana,
na hata yeye alifanya kazi nzuri hapa, alikuwa busy sana, namimi
nilikuwa busy ya studio. Unajua anakuta foleni kila siku halafu wewe
unapiga kazi kama masaa 15 hivi and then unachoka sasa huwezo kuongea
vizuri. Hata Saraha alichoka, unajua tulishindwa kuongea vizuri na kitu
kiliendelea. And then tulipofika Sweden, unajua upendo uliisha tu,
uliisha kabisa,” aliongeza.
Samwel ambaye tayari amerejea kwao nchini Sweden amesema yupo Tanzania kwa wiki
mbili kutengeneza nyimbo kadhaa.
No comments:
Post a Comment